TAARIFA KWA UMMA
Kuna hii taarifa upande wa kushoto iliyotengenezwa kwenye mfumo wa sauti na mwanamke na inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Jeshi la Polisi linaendelea kueleza katazo la kutokufanyika kwa kinachoitwa maandamano ya amani lililo tolewa jana Disemba 5,2025 lipo pale pale kwa sababu za kisheria ambazo hazijafuatwa na mbinu za kihalifu zinazopangwa sambasamba na maandamano hayo.Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi wakatae uhamasishaji, uzushi na uchonganishi wa aina hii na mwingine ambao lengo lake ni kuleta vurugu itakayo vuruga amani na usalama wa taifa letu.
Aidha, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vinaendelea kuwahakikishia wananchi wote wafuata sheria, wapenda amani, usalama wa taifa letu na wasiopenda kuchonganishwa na wanaopenda kutatua changamoto kwa busara, mazungumzo, maridhiano, maelewano na mshikamano wa kitaifa kuwa vipo tayari wakati wote kuwalinda siku zote.
Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania