DOHA-Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala yasiyo ya kijinai Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU-ADNA),Bi.Tabu Mzee amewasilisha Taarifa ya Tanzania kuhusu namna ilivyopiga hatua katika masuala ya urejeshwaji mali pamoja na ushirikiano wa kimataifa.
Akiwasilisha taarifa hiyo leo Desemba 18,2025,Bi.Tabu amesema, pamoja na mambo mengine, Tanzania imetekeleza vema Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa (UNCAC) kwa kufanya mambo mbalimbali.
Mosi ni Tanzania kuboresha sheria zinazohusu urejesheji mali ambazo ni Proceeds of Crime Act na Prevention and Combating of Corruption Act.
Pili, ni kumeimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa kuingia Mikataba ya Ushirikiano (MoUs) na mamlaka mbalimbali za kupambana na rushwa duniani.
Tatu, amesema, Tanzania imepokea na kuwasilisha maombi rasmi na yasiyo rasmi ya msaada wa kisheria (MLAs).
Akihitimisha taarifa hiyo, Bi.Tabu ameeleza, dhamira ya Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na mamlaka za kupambana na rushwa pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha kuwa kero ya rushwa inadhibitiwa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.
