KATAVI-Wananchi wa Kata ya Mwamkulu Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu waliopo katika maeneo yao ili kuimarisha usalama na kudumisha amani katika jamii.
Wito huo umetolewa leo Disemba 12, 2025 na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Katavi, Mrakibu wa Polisi John Mwaipungu wakati akitoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya uhalifu, ikiwemo kutoa taarifa mapema wanapobaini viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama katika maeneo yao.
SP. Mwaipungu amesisitiza kuwa ushirikiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi ni msingi muhumu wa kuimarisha ulinzi shirikishi akiwataka wananchi kuendelea kuwa walinzi wa kwanza wa maeneo yao na kutofumbia macho vitendo vya kihalifu vinavyojitokeza.


