Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza mwakani

DAR-Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesaini hati ya Makubaliano ( MoU) na Kampuni ya Africa Global Logistics ( AGL) Tanzania Ltd yenye Makao Makuu yake Nchini Ufaransa ambayo ni kampuni tanzu ya MSC, kwa ajili ya usanifu, Ujenzi na uendeshaji wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo.
Hati hii ya makubaliano (MoU) imesainiwa tarehe 6 Disemba,2025 Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa na Rais wa AGL Philippe Labonne.

Bw. Mbossa amesema, kusainiwa kwa hati ya Makubaliano ni ishara ya utayari wa kuanza kwa mradi wa Bandari mpya ya Bagamoyo ambapo kwa kuanzia AGL itaanza usanifu na Ujenzi wa gati tatu mpya za Kisasa kati ya 28 zinazotatajiwa kujengwa katika Bandari hiyo pamoja na gati mbili mpya za Kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Rais wa AGL Bw. Philippe Labonne anasema wameamua kuingia makubaliano na TPA na kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa nchi yenye Amani, Usalama na mazingira bora na tulivu ya uwekezaji iliyosehemu sahihi kijiografia kwa Sekta ya Uchukuzi na kuwa lango la Biashara Kitaifa na kimataifa.

Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa gati mpya tatu utajengwa kwa miezi 36 ( miaka mitatu) na Kampuni ya AGL imepata nafasi hii ya kushirikiana na TPA katika ujenzi huo kutokana na uzoefu wao kama kampuni kubwa ya huduma za usafirishaji na logistiki, inayotoa huduma kamili za usafirishaji, usimamizi wa mizigo, usafirishaji wa kimataifa na huduma za forodha, ikihudumia sekta mbalimbali kama uchimbaji, mafuta, chakula, na misaada ya kibinadamu, ikiwa sehemu ya kundi la kimataifa la AGL (zamani Bolloré T&L) na sasa wakiwa chini ya MSC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news