RUVUMA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa Kushirikiana na maafisa na askari toka vyombo vya ulinzi na Usalama Ruvuma limefanya matembezi (Route match) na mazoezi ya pamoja kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri baina ya Majeshi pamoja na kuimarisha afya ya mwili na akili.
Matembezi hayo yamefanyika Disemba 04, 2025 katika maeneo yote ya Manispaa ya Songea na viunga vyake yakihusisha matembezi na kukimbia baina ya askari hao.
Mazoezi na kushirikiana baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma imekuwa ni desturi lengo likiwa kuwaakutanisha pamoja na kubadilishana mambo mablimbali ya kiutendaji na kuwa tayari kukabiliana na changamoto yoyote itakayotokea mbele yetu.













