TANGA-Wananchi wa Kijiji cha Kitivo, Kata ya Lushoto, Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani na usalama katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa Desemba 25,2025 na Inspekta Karim Bruno, wakati wa zoezi la ushirikishaji jamii lililofanyika katika Kitongoji cha Kitivo, Kata ya Lushoto, Wilaya ya Lushoto.
Katika utoaji wa elimu hiyo, wananchi wameaswa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mara moja pindi viashiria vinapojitokeza, kupinga vikali ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto, pamoja na kuacha kujihusisha na biashara haramu za pombe aina ya moshi na dawa za kulevya ikiwemo bangi.
Wananchi wa Kijiji cha Kitivo wameishukuru Jeshi la Polisi kwa elimu waliyopewa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Polisi katika kulinda amani na usalama wa maeneo yao.


