WASHINGTON D.C (15 Desemba,2025)-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amekutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Florida kutoka Chama cha Republican, Mhe. Brian Mast na kukubaliana kuimarisha na kukuza ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani.
Aidha, Mhe. Waziri Kombo pia amekutana na kufanya mazungumzo na wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani na wadau wengine kwa madhumuni ya kuimarisha ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.



