Waziri Mavunde,Perseus wajadili maendeleo Mradi wa Nyanzaga

DAR-Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Desemba 2, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni mama ya Perseus na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga, Bi. Lee-Anne de Bruin ambao ni wawekezaji kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo wilayani Sengerema.
Bi. Lee-Anne de Bruin aliongozana na Bw. Matt Cavedon, Meneja Mkuu na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga na Bw. Isaac Lupokela, Afisa Mkuu wa Fedha wa Mradi wa Nyanzaga.
Mazungumzo hayo yaliangazia hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa uanzishwaji wa mgodi huo ambao unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu na wananchi wa Sengerema.
Aidha, Waziri Mavunde amewahakikishia wawekezaji wa Perseus kuwa wizara itaendelea kuwa bega kwa bega na wawekezaji katika kufanikisha uendelezaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Nyanzaga ili uweze kuleta mafanikio kwenye uchumi wa Tanzania na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa Watanzania wengi.

#InvestInTanzania

#Vision2030:Madini ni Maisha&Utajiri

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here