DODOMA-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwa niaba ya Serikali,inapenda kuufahamisha umma kuwa Serikali ya Marekani imetangaza kuiweka Tanzania katika kundi la nchi 15 ambazo Serikali hiyo imedhibiti utaratibu wa visa (partial restrictions) za kuingia nchini humo.
Uamuzi huo umetangazwa na Rais wa Marekani, Mhe. Donald Trump, tarehe 16 Desemba 2025, na unahusisha pia nchi nyingine 14 ambazo ni Angola, Antigua and Barbuda, Benin, Cote d’Ivoire, Dominica, Gabon, Gambia, Malawi,Mauritania, Nigeria, Senegal, Tonga, Zambia na Zimbabwe.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi la Serikali ya Marekani, udhibiti huo umetokana na taarifa ya Wakaaji Zaidi ya Muda (Overstay Report), iliyoonesha kuwepo kwa idadi ya baadhi ya raia wa Tanzania waliokwenda nchini Marekani na kuzidisha muda wa kukaa kinyume na masharti ya viza walizopewa.
Taarifa hiyo imeonesha kuwa Tanzania ina kiwango cha ukaaji wa zaidi ya muda cha:
• Asilimia 8.30 kwa viza za B-1/B-2 (biashara na utalii); na
• Asilimia 13.97 kwa viza za F, M na J (wanafunzi, mafunzo ya ufundi na programu za kubadilishana).
Kwa mujibu wa Serikali ya Marekani, viwango hivyo vilionekana kuzidi kiwango kinachokubalika chini ya sera zao za uhamiaji, na hivyo kusababisha Tanzania kujumuishwa katika kundi la nchi zilizowekewa udhibiti huo.
Serikali ya Marekani imeeleza kuwa, udhibiti huu si kamili na kwamba Watanzania watakaokidhi vigezo na masharti ya uhamiaji wataendelea kuruhusiwa kuingia nchini Marekani, kulingana na taratibu na;

