ROME-Januari 8,2026 Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani,Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua aliyekuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Arusha, Mhashamu Prosper Baltazar Lyimo kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Bariadi.
Askofu Lyimo alizaliwa Agosti 20, mwaka 1964 ambapo baada ya masomo ya kipadri alipewa Daraja Takatifu la Upadre mnamo Julai 04 mwaka 1997 jimboni Arusha.Askofu Lyimo ambaye ana shahada ya uzamivu (PhD) katika sheria za Kanisa, alikuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Arusha tangu mwaka 2015.
Tarehe ya kusimikwa rasmi kwa Askofu Lyimo kuwa Askofu wa kwanza na mwanzilishi wa Jimbo jipya la Bariadi, itatangazwa hapo baadaye.
Tags
Askofu Prosper Lyimo
Breaking News
Habari
Kanisa Katoliki Duniani
Kanisa Katoliki Tanzania
Papa Leo XIV
