DAR-Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa, amesaini Kitabu cha Maombolezo, katika Ofisi za Ubalozi wa Yemen nchini Tanzania jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa zamani wa Yemen Kusini na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Yemen, Hayati Ali Salem al-Beith.
Akiwasilisha salaam za rambirambi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mussa amesema Tanzania imepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo, na inaungana na familia ya marehemu Ali Salem al Beidh, katika maombolezo.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa pole za dhati kwa familia ya marehemu na inashirikiana na Serikali na watu wa Yemen katika kipindi hiki kigumu’ alieleza Balozi Mussa.



