TANGA-Bodi ya Bima ya Amana (DIB) inashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Usagara jijini Tanga yakijumuisha wizara na taasisi mbalimbali za fedha zinazotoa huduma hizo hapa nchini.
Pichani maafisa wa DIB wakitoa elimu kuhusu majukumu ya DIB kwa wanafunzi wa Chuo cha Kange waliotembelea banda la DIB.
Maonesho haya ambayo yalianza tarehe 19 Januari 2026 yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 21 Januari na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni: “Elimu ya Fedha, msingi wa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.”
