DAR-Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kumekuwepo taarifa za upotoshaji zinazosambazwa na watu wasiokitakia mema chama hicho zikiwahusisha viongozi wa chama na kashfa zinazohusisha madai ya michango iliyoendeshwa hivi karibuni mtandaoni ili kumchangia Mwenyekiti wa chama,Tundu Lissu.
Mkurugenzi wa Mawasialiano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi.Brenda Rupia.
Katika taarifa iliyotolewa Januari 29,2026 na chama hicho, CHADEMA kimesema, "Tunapenda kutoa ufafanuzi kwamba, michango kwa ajili ya Mwenyekiti wa Chama Taifa iliratibiwa kupitia namba ya simu ya ndugu yake Wakili Alute Mughwai Lissu.
"Aidha, uratibu na upokeaji wa michango hii haukufanywa na Sekretarieti ya chama Taifa au na kiongozi yoyote wa chama.
"Tunawaomba Watanzania na dunia nzima kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa kwa lengo la kuchafua taswira ya chama na viongozi wake."

