OSG yajipanga uendeshaji wa majukumu ya kisheria

DODOMA-Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yafanya tathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha nusu Mwaka wa Fedha 2025/26 na kujipanga kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha mwezi Januari, 2026 hadi Juni, 2026.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiendesha kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi ameendesha kikao cha menejimenti cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuchambua taarifa ya utekelezaji ya Ofisi hiyo, kupanga mikakati mipya ya utendaji kazi ili kuhakikisha kuwa Ofisi hiyo inaendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa tija na ufanisi ndani na nje ya nchi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akifuatilia majadiliano ya kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.

“Kikao hiki ni cha kimkakati, lengo ni kujipanga kuendesha majukumu ya kisheria ya Ofisi ikizingatiwa kuwa kikao hiki kinafanyika kuelekea Siku ya kilele cha Wiki ya Sheria inayoadhimishwa kila mwaka mwanzoni mwa mwezi Februari, 2026,” amesisitiza Dkt. Possi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Asha Hayeshi akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Idara hiyo kwenye kikao cha menejimenti ya Ofisi hiyo cha kutathmini utendaji kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakijitambulisha kabla ya kikao cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiendesha kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha menejimenti ya Ofisi hiyo cha kutathmini utendaji kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiendesha kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.

Pia, Dkt. Possi ameongeza kuwa Ofisi imedhamiria kufungua Ofisi nyingine kwenye mikoa ya Katavi, Geita, Singida ili kusogeza huduma karibu na wananchi na amewataka wajumbe wa menejimenti ya Ofisi hiyo kuendelea kutumia mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyesimama katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo kabla ya kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi hiyo, Bi. Asha Hayeshi.

Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akizungumza kwa niaba ya menejimenti ya Ofisi hiyo amemhakikishia Dkt. Possi kuwa kwa kuwa mwaka mpya umeanza na Ofisi inaingia kipindi cha pili cha Mwaka wa Fedha, wajumbe wa menejimenti hiyo wataendelea kutekeleza majukumu kwa wakati.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyesimama katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kikao cha kutathmini utendaji kazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo.

Kikao hicho hufanyika mara moja kwa mwaka ili kuwapa muda wa kutosha wajumbe wa menejimenti wa Ofisi hiyo kutoa taarifa ya utendaji kazi na majukumu yaliyopangwa kutekelezwa kwa kipindi cha pili cha Mwaka wa Fedha 2025/26.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here