Dkt.Akwilapo aongoza watumishi Ardhi kupanda miti Mtumba jijini Dodoma

DODOMA-Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo na Naibu wake Mhe. Kaspar Mmuya leo Januari 27, 2026 wamewaongoza watumishi wa Wizara katika zoezi la upandaji miti kwenye Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni siku ya kitaifa ya kuhamasisha upandaji miti.
Zoezi hilo linaongozwa na Kaulimbiu “Kesho yetu inaanza na mti unaopandwa leo, Panda mti kwa maendeleo endelevu ya makazi.”
Katika kufanikisha zoezi hilo,viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi, Vyuo vya Ardhi Morogoro (ARIMO) na kile cha Tabora (ARITA) pamoja na Ofisi za Ardhi za Mikoa zimeelekezwa kushiriki zoezi hilo kwa kupanda miti kwenye maeneo yao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema, wizara yake inashiriki zoezi la upandaji miti kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwana mazingira namba moja kutunza mazingira hasa ikizingatiwa kuwa leo Januari 27, 2026 ni siku yake ya kuzaliwa.
Waziri huyo wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewahamasisha watumishi wa sekta ya ardhi nchini pamoja na wananchi kwa ujumla kukumbuka kuwa miti ni uhai hivyo wapande miti na kuitunza kwa lengo la kumuunga mkono Rais akiwa mwanamazingira namba moja.

”Wakati tunasherekea siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais, yeye ni mwana mazingira namba moja tunamuunga mkono kwa vitendo kwa kuhakikisha tunapanda miti ikiwa ni juhudi za kutunza mazingira,’’amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa hiari wakitambua kuwa ulinzi wa mazingira ni msingi wa uhai, maendeleo na Usalama wa taifa.

Zoezi hili ni ishara ya uwajibike na linatoa fursa kwa kila mmoja kwa nafasi na mahali alipo kushiriki katika kulinda na kuenzi mazingira kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here