Fundi seremala kizimbani kwa kumshambulia mke wake

MWANZA-Hamza Omary (38), fundi Seremala na mkazi wa Luchelele, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Mkuyuni, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Januari 19, 2026, akikabiliwa na shtaka la kumshambulia mke wake katika Kesi ya Jinai namba 75/2026.
Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 07, 2026 katika eneo la Luchelele, Mtaa wa Kisoko, majira ya saa 3.30 usiku, ambapo alimshambulia mke wake aitwaye Anna Zacharia kwa kumpiga ngumi, kumrushia sufuria kichwani na kumng’ata mkono wa kushoto.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni, Mhe. Witness Ndosi, Mwendesha Mashtaka Koplo Dorothy Mauma alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 240 cha Sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Marejeo ya mwaka 2023.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na amepelekwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Masharti ya dhamana yalikuwa ni kuwa na mdhamini mmoja, barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata pamoja na fungu la dhamana la ahadi kiasi cha shilingi laki moja (100,000) tu. Mhe. Witness Ndosi ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 02,2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here