MORONI-Ubalozi wa Tanzania umeratibu utekelezaji wa mkataba wa Kampuni ya Kitanzania ya Afrifeed Holdings Ltd na Manispaa ya Moroni ambapo Kampuni hiyo imekabidhi gari maalum aina ya Wheel Loader ili kusaidia utunzaji wa mazingira katika Manispaa hiyo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano Balozi wa Tanzania nchini humo,Saidi Yakubu amesema kuwa, mapema mwezi Septemba ubalozi uliratibu majadiliano yaliyofikia kusainiwa mkataba wa ushirikiano baina ya Kampuni ya Kitanzania na Manispaa ya Moroni ambapo katika mkataba huo ilikubaliwa kampuni hiyo kutoa gari la kukusanyia taka na lori la kuzibeba na wao wataruhusiwa kukusanya taka ngumu za chuma katika mji huo ikiwemo magari chakavu.
Aidha, alieleza kuwa uwepo wa mradi huo Comoro utasaidia pia kutoa ajira na mapato kwa ushuru na kodi zitakazolipwa.Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani anayeshughulikia pia Serikali za Mitaa,Mheshimiwa Mohamed Ahamada.
Meya wa Manispaa hiyo,Omari Mohamed alisema kuwa hatua hiyo itaimarisha juhudi zao za kutunza mazingira na kuchochea ajira katika mji wao.



