Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara yatajwa kuwa bora zaidi barani Afrika

DAR-Ligi Kuu ya NBC imeendelea kuwa miongoni mwa Ligi 10 Bora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).
Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa juma hili,Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inashika nafasi ya sita (6) kwa ubora barani Afrika na ya 54 duniani.

Licha ya kushuka kwa nafasi mbili (2) Afrika ikilinganishwa na mwaka 2024, Ligi yetu imepanda kwa nafasi tatu (3) duniani, kutoka nafasi ya 57 (2024) hadi nafasi ya 54 (2025) na alama zimeongezeka kutoka 266.75 (2024) hadi 308.5 (2025).

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imewashukuru wadau wote wa Ligi hii kwa jitihada zilizofanya Ligi yetu iendelee kuwa miongoni mwa Ligi Bora na zenye mvuto barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here