Magazeti leo Januari 22,2026

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kambi maalum ya matibabu ya kisasa ya upasuaji wa kuondoa mawe kwenye figo kwa wagonjwa wenye changamoto hiyo kwa kutumia njia ya kisasa ya mionzi ya laser.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Mfumo wa Mkojo wa MNH -Mloganzila, Dkt. Hamis Isaka ameeleza kuwa, kambi hiyo ambayo imeanza Januari 21 hadi 23, 2026 inafanywa na wataalamu wa ndani waliobobea katika upasuaji wa mfumo wa mkojo.
Amefafanua kuwa, kutokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa wananchi wengi, hospitali imeamua kutoa matibabu hayo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji mkubwa uliyofanywa na Serikali katika sekta ya afya .

Kwa mujibu wa Dkt.Isaka huduma ya kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mionzi ya Laser ni matibabu ambayo humsaidia mgonjwa kupata maumivu kidogo,kutokuwa na kovu wala kukatwa ambapo mgonjwa atakaa wodini kwa siku mchache takribani siku moja hadi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here