MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imefafanua kuwa dawa maarufu ya P2 haitumiki kutoa mimba kama ilivyovipotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na badala yake hutumika kuzuia mimba kutunga kabla ya saa 72 ya kufanya tendo la ndoa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo imeeleza kuwa matumizi ya dawa hiyo zenye kiambata hai (active ingredient) kijulikanacho kama ‘levonorgestrel’ imethibitishwa na TMDA kutumika kama mojawapo ya njia za uzazi wa mpango na hutakiwa kutumika ndani ya masaa 72 baada ya tendo la ndoa."Taarifa iliyorushwa hewani na baadhi ya vyombo vya habari vikinukuu matumizi holela ya dawa husika ambayo ilionesha kuchanganya maelezo ya dawa za aina mbili tofauti ambazo zilikuwa zikizungumziwa kwa wakati mmoja.Katika taarifa hiyo iliyojichanganya ilionekana kuainisha kwamba dawa P2 hutumika kwa ajili ya kutoa mimba,” imeeleza taarifa hiyo.
"Taarifa sahihi ni kwamba dawa zenye kiambata cha levonorgestrel zinatumika kuzuia mimba baada ya kufanya tendo la ndoa na kuwa na wasiwasi wa kupata ujauzito kwa dharura”.
Pamoja na ufafanuzi amesema matumizi ya P2 madhara yake ni pamoja na kuharibu mzunguko wa hedhi, kupata hedhi nyepesi au nzito, kuwahi au kuchelewa kupata hedhi, maumivu ya tumbo, kuharisha, kizunguzungu, kuchoka, kupata gesi tumboni na kuumwa kichwa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















