WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema kuwa katika siku 100 za kwanza za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha pili cha uongozi, Wizara hiyo imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 821.7, hatua iliyochangia kuanzishwa kwa viwanda vidogo na kuzalisha ajira 546 za moja kwa moja, zikiwemo ajira 436 kwa vijana.
Ameyasema hayo Januari 24,2026 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia katika sekta ya Viwanda na Biashara ndani ya siku 100 za kwanza za Awamu ya Sita katika kipindi cha pili cha uongozi wake.Amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika uendelezaji wa mitaa ya viwanda, baada ya kukamilisha tathmini ya awali ya kongani za viwanda katika mikoa 11 nchini, pamoja na kuandaa maeneo manne ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwa ajili ya uzinduzi rasmi, hali iliyoanza kuzalisha maelfu ya ajira, nyingi zikiwa ni za vijana.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo









