Familia ya Juma Maganga imemshukuru Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Mtumba, Mhe. Anthony Mavunde kwa kumsaidia mtoto wao kuachiwa huru kufuatia tukio lililotokana na ajali ya barabarani.
Ajali hiyo ilitokea Februari 14,2025 nchini Sudan Kusini, ambapo Juma Maganga, aliyekuwa dereva wa gari kubwa, alimgonga mwanajeshi mmoja aliyepoteza maisha. Tukio hilo lilisababisha Juma kushikiliwa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo.
Juma Maganga alitakiwa kufanya malipo ya dola za Kimarekani 1,500 katika Mahakama ya Juba, Sudan Kusini. Desemba 29,2025, Mhe. Anthony Mavunde alifanikisha hatua hiyo ya malipo, hatua iliyofungua njia ya kuachiwa kwa Juma Maganga.
Aidha,Desemba 31,2025, Juma Maganga aliachiliwa huru na kuanza safari ya kurejea nyumbani Dodoma, Tanzania ambapo aliwasili Januari 3,2026 na kupokelewa nyumbani.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo








