Mheshimiwa Balozi Omar akagua jengo jipya la kisasa la ofisi za Wizara ya Fedha

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Jengo jipya la kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, litawawezesha watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi katika mazingira bora na kuwahudumia wananchi na wadau wake wengine kwa ufanisi zaidi.
Muonekano wa Mandhari ya Jengo jipya la Kisasa la Wizara ya Fedha, lililopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, ambalo Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amelitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wake ambao umekamilika kwa asilimia 98, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Mhe. Balozi Omar, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo akiambatana na Naibu Mawaziri wake wawili, Mhe. Larent Luswetula, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, na Menejimenti ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiweka kadi katika mfumo wa usalama na utambuzi iliyopo katika Jengo Jipya la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, ili kumruhusu kuingia, wakati alipotembelea na kukagua Jengo hilo jipya la Ofisi la Kisasa lenye ghorofa 9 kisasa, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiongea jambo wakati akikagua eneo la Mgahawa katika Jengo Jipya la Kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (mwenye shati ya njano), akisikiliza maelezo kuhusu eneo la lifti na matumizi yake kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi wa Jengo la Wizara ya Fedha, Mhandisi. Japhet Mkwamira (kushoto), wakati akikagua Jengo jipya la kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa pili kushoto) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (wa tatu kushoto). Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (watatu kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia).
Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha jengo hilo kujengwa na kukamilika.

Mhe. Balozi Omar, amewataka watumishi wa wizara hiyo kulitunza jengo hilo na kuhakikisha kuwa mifumo yake ya ulinzi na usalama inasimamiwa ipasavyo.
Wakizungumza katika ziara hiyo, Naibu Mawaziri, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) na Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), walisema kuwa Jengo hilo ni la kisasa na limejengwa kwa viwango vya hali ya juu.

Akitoa taarifa wa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo kutoka Wizara ya Fedha, Mhandisi Japhet Mkwamira, alisema kuwa ujenzi wa Jengo lenye ghorofa 11 ambalo ni Jengo refu kuliko majengo yote ya Serikali yaliyopo Mji wa Serikali-Mtumba kwa sasa, limekamilika kwa asilimia 98.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa tisa kushoto) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (wa tisa kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nane kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nane kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa Wizara ya Fedha baada ya kukagua Jengo jipya la kisasa la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma.
Jengo hilo la Wizara ya Fedha, linajengwa na Mkandarasi Mkuu Kampuni ya Estim Construcion Co. Ltd, na Mshauri Elekezi wa mradi, ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likishirikiana na IPA Architects Ltd katika Usanifu na Usimamizi wa ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here