Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Januari 19,2026

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Young Africans (Yanga SC) imeendelea kuonesha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 baada ya kujikita kileleni mwa msimamo mwa ligi, ikikusanya pointi 19 katika michezo saba.

Yanga imeshinda mechi sita na kutoka sare moja bila kupoteza mchezo wowote, ikiwa na rekodi bora ya mabao 18 ya kufunga dhidi ya bao moja pekee iliyoruhusu, hali inayoipa tofauti ya mabao 17, bora zaidi hadi sasa.

Aidha,nafasi ya pili inashikiliwa na JKT Tanzania yenye pointi 17 baada ya kucheza michezo 10, ikifuatiwa na Pamba Jiji iliyo katika nafasi ya tatu kwa pointi 16.
Kwa upande wa Simba SC ipo nafasi ya nne kwa pointi 13, ikiwa imecheza michezo sita na kuonesha ushindani mkali katika mbio za kuwania nafasi za juu.

Mashujaa FC na Azam FC zinashika nafasi ya tano na ya sita kwa pointi 13 na 12 mtawalia, huku Namungo FC na Mtibwa Sugar zikiendelea kusaka uthabiti katikati ya msimamo wa ligi.

Katika eneo la hatari,Dodoma Jiji ipo nafasi ya 15 kwa alama saba baada ya mechi tisa, huku KMC FC ikiburuza mkia wa ligi kwa pointi nne baada ya michezo tisa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here