NA DIRAMAKINI
CHUO cha Ufundi Arusha (ATC) kimetangaza kufuta rasmi Mahafali ya mwaka 2025 yaliyopangwa kufanyika Januari 31, 2026, kutokana na idadi ndogo ya wahitimu waliothibitisha kushiriki na kulipia mavazi ya mahafali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 29, 2026 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Gasto John Leseiyo, ni asilimia saba tu ya wahitimu 908 waliolipia mavazi ya mahafali, hali iliyofanya tukio hilo kuwa gumu kutekelezeka kiuchumi.
Taarifa ya Chuo imeeleza kuwa Wahitimu waliolipia wanatakiwa kuwasilisha maelezo yao kwa ajili ya kurejeshewa fedha kabla ya Januari 30, 2026.
ATC imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwataka wahitimu kuwa wavumilivu na kushirikiana kwa uelewa.
.jpeg)
