NA DIRAMAKINI
JESHI la Polisi limesema limeanza kuchunguza wa kina picha mjongeo ambayo inaonesha watu wawili wakipigwa kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na haki za binadamu.
Jeshi hilo limesema uchunguzi huo umeanza ili kubaini anayefanya kitendo hicho ni nani, wanaofanyiwa ukatili huo ni akina nani, ulifanyikia wapi na lini ili hatua stahiki na za haraka za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhusika.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za kuweza kusaidia kumbaini aliyekuwa anafanya ukatili huo, atoe ushirikiano.
Pia, waliokuwa wanafanyiwa ukatili huo nao wajitokeze kwa kiongozi yeyote wa Polisi au kwa watakayemwona ni rahisi kwao ili kufanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa anawafanyia kitendo hicho kilicho kinyume na sheria.
