ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 13 Januari 2026, amevizindua rasmi Viwanja vya Michezo vya Gombani vilivyopo Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Uzinduzi wa Viwanja vya Michezo vya Gombani umefuatiwa na Mchezo wa Fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026 uliozikutanisha klabu kongwe za soka nchini, Azam FC na Yanga SC, mchezo uliovutia maelfu ya mashabiki wa soka kutoka ndani na nje ya Zanzibar.
Uwanja wa Gombani umefanyiwa ukarabati nkubwa na Kampuni ya Reform Sports pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Wilaya ya Chakechake na kiwanja cha Michezo mingine ikiwemo Mpira wa Mikono, Mpira wa Wavu na Mpira wa Kikapu pembezoni mwa Uwanja wa Mkubwa wa Gombani.
Uzinduzi huo ni Miongoni mwa Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


















