REA yamtaka Mkandarasi Northern Engineering Mtwara kuongeza kasi utekelezaji wa mradi

MTWARA-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 150 vya Majimbo 10 mkoani Mtwara kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha mradi kwa wakati.
Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme REA, Mha. Deogratius Nagu ametoa maelekezo hayo Januari 29, 2025 kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi katika Wilaya za Nanyumbu, Newala, Tandahimba na Masasi Mkoani Mtwara.

"Kasi ya utekelezaji wa mradi hairidhishi, jitahidini kuongeza kasi, tafuteni watoa huduma wa vifaa wengi ili ikitokea mmoja kachelewa mnachukua kwa mwingine," alielekeza Mha. Nagu.
Alisema, kutegemea mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila kifaa ni jambo la hatari kwani ikitokea amechelewa kugikisha vifaa site, kazi zinasimama na kuchelewesha kukamilika kwa mradi na aliwasisitiza kufanya kazi na Watoa huduma wanaotambuliwa na walio katika kanzidata za TANESCO ili kupata vifaa vyenye ubora unaokubalika.

Mha. Nagu alisema Mkandarasi wa Mradi Kusambaza Umeme atakayefanya vizuri anayo nafasi kubwa ya kupata kazi ya kutekeleza mradi mwingine.

"Mnapaswa kuwasimamia kwa karibu hawa wanaowasambazia vifaa mathalani huyu anayewauzia transfoma, hakikisheni mnaweka mtu wenu maalum kiwandani kwa ajili ya kufuatilia kukamilika kwa taratibu za kusafirisha transfoma hizo kuja site," alielekeza Mha. Nagu.
Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Nothern Engineering, Mha. Christopher Masasi alikiri kuwepo kwa changamoto ya kucheleweshewa vifaa kutoka kwa watoa huduma na aliahidi kuongeza idadi ya watoa huduma watakosambaza vifaa kwa ajili ya mradi.

"Ni kweli hatuna changamoto zaidi ya hii ya kucheleweshewa vifaa na watoa huduma, tumepokea maelekezo na tunaahidi kuongeza kasi na leo hii tumepokea shehena ya vifaa hivyo kasi itaongezeka," alisema Mha. Masasi.
Aidha, kwa mujibu wa Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoani Mtwara, Mha. Daniel Mwandupe amesema Mkandarasi Nothern Engineering Works Limited anatekeleza mradi wenye thamani ya shilingi 16,717,407,821.65 utakaonufaisha Kaya 4,950.

Mha. Mwandupe amesema hadi sasa Mkandarasi amewasha vitongoji 40 na kuunga wateja 458 na anatarajiwa kukamilisha mradi ifikapo Agosti mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here