Serikali yatoa shilingi bilioni nne kugharamia matibabu ya upasuaji wa Mabusha nchini

DAR-Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni Nne (4) kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa Mabusha nchini ambapo wananchi wanapata huduma hiyo bila malipo.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema hayo alipofanya ziara kwenye kambi ya upasuaji Mabusha katika Kituo cha Afya Kilakala, Temeke Jijini Dar es Salaam zoezi linaloendelea kwa wiki tatu.

"Serikali imegharamia zaidi ya Shilingi Bilioni Nne katika huduma hii ambapo Upasuaji huu unafanyika kwa kitaalamu, mgonjwa anapewa dawa za usingizi tu sehemu ambayo anafanyiwa upasuaji na ufahamu wake unakuwa upo kama kawaida na," amesema.

Aidha, Dkt. Magembe amesema tangu kambi za upasuaji wa Mabusha katika Mkoa wa Dar es Salaam zianze, zaidi ya watu 1300 wamejitokeza ambapo upasuaji wa Mabusha umefanyika kwa watu 668 na lengo lilikuwa ni watu 5000 kwenye kituo cha afya Kilakala na Kinondoni.

"Ili kujikinga na magonjwa haya ni muhimu kuzingatia usafi wa mazingira ikiwemo kufukia madimbwi ya maji, kufyeka nyasi katika maeneo yanayotuzunguka ili kuzuia mazalia ya Mbu," amesema.

Pia, Dkt. Magembe ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi juu ya umuhimu wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote kufuatia utekelezaji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohammed Mang'una amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo kwa kuwa zinatolewa bila malipo ambapo Takwimu zinaonesha kuwa wanaojitokeza zaidi ni wenye umri zaidi ya miaka 45.

Kambi hiyo inafanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo pia itaendelea katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Morogoro pamoja na Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here