Serikali yawafariji wananchi walioathiriwa na mafuriko wilayani Kilosa

KILOSA-Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu),Dkt.James Kilabuko leo Januari 1, 2026 ametembelea kambi maalum iliyotengwa kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika Kitongoji cha Mateteni na Legeza Mwendo, Kata ya Tindiga Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Akiwa katika Shule ya Msingi Tindiga, Dkt. Kilabuko ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa,Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka pamoja wataalam mbalimbali kutoka wilayani Kilosa.
Dkt.Kilabuko amewapa pole wananchi hao na kuwahakikishia kuwa, Serikali ipo pamoja nao katika hali zote.

Ikumbukwe mnamo usiku wa kuamkia Desemba 26, 2025 mvua kubwa iliyonyesha katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kilosa ilisababisha mafuriko na kuharibu miundombinu mbalimbali na makazi ya watu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here