Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tunapenda kuwashukuru wadau wetu na wananchi kwa ujumla, kwa ushirikiano mkubwa mliotupatia katika kipindi chote cha mwaka 2025.
Ushirikiano wenu na imani yenu kwetu, ndiyo iliyotuwezesha kuendelea kutoa huduma bora za Ushauri wa Kisheria,Upekuzi wa Mikataba na Uandishi wa Sheria.
Tunapouanza mwaka mpya wa 2026, tunawaahidi kuendelea kuwahudumia kwa Weledi wa hali ya juu.
Ahsanteni kwa kuwa sehemu ya safari yetu kwa mwaka 2025. Karibuni tujenge mwaka 2026 uwe wa mafanikio zaidi.
