Tanzania yaongoza kwa ukuaji wa huduma za usafiri kwa mitandao barani Afrika

DAR-Kampuni ya Bolt imetoa ripoti yake ya kimataifa ya takwimu za usafiri, ikionyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa masoko yanayokua kwa kasi duniani na kinara barani Afrika kwa ongezeko la safari kwa mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu za 2025, matumizi ya Bolt nchini Tanzania yameongezeka kwa asilimia 68, kiwango kilichozipiku Kenya (+35%), Afrika Kusini (+25%), Nigeria (+3%) na Ghana (+2%).

Takwimu hizo pia zinaonesha Tanzania ikiungana na masoko ya juu duniani kama Uswisi (+173%), Norway (+45%), Slovakia (+37%) na Ubelgiji (+37%) kama miongoni mwa masoko yanayokua kwa kasi zaidi duniani.

Kwa ujumla, Bolt imerekodi ongezeko la asilimia 46 ya safari duniani, ikichochewa na ongezeko la matumizi ya teknolojia na ufanisi wa huduma katika Ulaya, Afrika na Asia.

Ukuaji wa Tanzania unahusishwa moja kwa moja na kupanuka kwa mazingira ya kidijitali nchini.

Takwimu za TCRA 2024/25 zinaonyesha matumizi ya intaneti yamefikia zaidi ya asilimia 72, huku usajili wa laini za simu ukifikia zaidi ya milioni 63, jambo linaloifanya simu kuwa njia kuu ya kupata huduma za mtandaoni.

Ripoti ya GSMA Mobile Economy Africa 2024 pia inaitaja Tanzania kama soko linalokua kwa kasi, ikiwa na ongezeko kubwa la utumiaji wa smartphone na watumiaji wa intaneti ya simu wanaotarajiwa kukua zaidi ya wastani wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Wachambuzi wa sekta wanaeleza kuwa, mabadiliko haya yamebadili mienendo ya usafiri mijini, hasa kwa vijana wanaopendelea huduma za mtandao kwa sababu ya usalama, uaminifu na uwazi wa bei.

Akizungumza kuhusu matokeo hayo, Meneja Mkuu wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, alisema ukuaji huo unaonesha uhai wa uchumi wa kidijitali nchini.

“Tanzania inaandika upya historia ya usafiri barani Afrika. Ukuaji huu ni ishara ya mahitaji ya usafiri salama na nafuu, lakini pia kasi ya kidijitali na ubunifu wa madereva wetu,” alisema.

Kuongezeka kwa matumizi ya huduma za kidijitali nchini kunaifanya Tanzania kuwa moja ya kitovu muhimu cha ukuaji wa huduma za usafiri kwa njia ya mtandao barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here