Tume yakanusha madai ya kumpekua DPP uhalali wa tuhuma zake

DODOMA-Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imekanusha taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Nipashe la tarehe 27 Januari 2026, ikisema kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haikutolewa na Tume hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jijini Dodoma, Tume imesema habari yenye kichwa cha “Tume ya Sheria yampekua DPP uhalali wa tuhuma zake” (Toleo Na. 0582294) inawasilisha taarifa zisizo sahihi na zinazoipotosha jamii. Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hiyo.

Tume imefafanua kuwa haina mamlaka ya kisheria ya kupekua, kuchunguza au kutathmini uhalali wa taasisi au afisa yeyote wa umma, ikiwemo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kama ilivyoelezwa kwenye habari hiyo.

Badala yake, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ina jukumu la kufanya tafiti, mapitio na tathmini ya sheria zilizopo ili kubaini mapungufu na kutoa mapendekezo ya maboresho ya mfumo wa sheria kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Aidha, Tume imevitaka vyombo vya habari kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, ikiwemo kuthibitisha taarifa kabla ya kuzichapisha, ili kulinda maslahi ya umma na kudumisha uaminifu wa habari.

Tume imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, za ukweli na zenye manufaa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here