PWANI-Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Agnes Amos Liku mwenye umri wa miaka 35 na Mkazi wa Mwanzo Mgumu katika Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa amejifungua mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Mwanzomgumu kisha mtoto wake akachukuliwa na Afisa Tabibu asiyefahamika.




