Waziri wa Fedha,Balozi Omar ashiriki maziko ya Edwin Mtei

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameshiriki katika Misa ya maziko ya aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, marehemu Edwin Isaac Mtei, yaliyofanyika nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha, ambapo katika Misa hiyo upande wa Serikali iliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiweka shada la maua katika kaburi wakati Misa ya maziko ya aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Marehemu Edwin Isaac Mtei, kama ishara ya kutoa heshima ya mwisho, yaliyofanyika nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha).
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akisaini kitabu cha maombolezo wakati alipofika kushiriki Misa ya maziko ya aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Marehemu Edwin Isaac Mtei, yaliyofanyika nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha.
Pia,marehemu Edwin Isaac Mtei amehudumu nafasi mbalimbali nje ya Tanzania kama Mkurugenzi wa Bodi wa Shirika la Fedha Duniani – IMF na pia Katibu Mkuu wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here