Askari 13 Ruvuma watunukiwa vyeti vya heshima

RUVUMA-Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas amewataka askari Polisi Mkoa wa Ruvuma kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia haki, weledi na uadilifu katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuweza kufikia lengo la Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo ameyasema Februari 14, 2026 katika Viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Ruvuma baada ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali waliofanya vizuri zaidi katika utendaji wa kazi wa kuimarisha Usalama wa raia na Mali zao kwa kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu katika kipindi cha mwaka 2025 ikiwa ni Maadhimisho ya Police Family day.
Sambamba na hilo, Mhe.Ahmed Abbas ametoa pongeza kwa askari wote Mkoani Ruvuma kazi nzuri wanazofanya kuhakikisha Mkoa wa Ruvuma unaendelea kuwa salama sanjari na kuwataka kuongeza jitihada zaidi katika utendaji wao wa kazi ili kutimiza dhima na lengo la Jeshi la Polisi Tanzania ya kutoa huduma bora kwa wananchi sambamba na kubaini na kutanzua vitendo na viashiria vyote vya uhalifu.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),Marco G. Chilya amesema kuwa zawadi hizo za heshima zilizotolewa ni chachu ya kutambua mchango na kazi nzuri zinazoendelea kufanywa na askari wote ambapo amewasisitiza kwenda kufanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka 2026 kana viapo vyinavyowaelekeza katika kutekeleza majukumu ya utendaji kazi kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Sanjari na utoajia wa zawadi hizo Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas akiongozwa na Kamanda wa Polisi Ruvuma,Marco G. Chilya (SACP) alipata wasaha wa kukagua Gwaride la heshima lililoandaliwa na Askari toka vitengo vyote Mkoani Ruvuma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here