Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Juhud Mkosa (30), mkazi wa Kijiji cha Kijombe, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi baada ya kumshutumu kuhusika na ushirikina uliodaiwa kusababisha mimba za mke wake kuharibika mara kwa mara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamouda Banga, amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa alitekeleza mauaji hayo Novemba 29, 2025, dhidi ya baba yake, Ernesto Mkosa. Amesema baada ya mahojiano, mtuhumiwa alikiri kutenda tukio hilo.Akizungumzia sababu ya tukio hilo, Kamanda Banga amesema mtuhumiwa alidai kuwa baba yake ndiye aliyekuwa akihusika na kuharibika kwa ujauzito wa mke wake kupitia vitendo vya ushirikina.
"Sababu halisi iliyopelekea mtuhumiwa huyu kutekeleza mauaji hayo ni kumtuhumu mzazi wake kwa ushirikina, akidai mke wake alikuwa akibeba ujauzito ambao ulikuwa ukiharibika mara kwa mara," amesema Kamanda Banga.
Kamanda Banga amesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea kukamilishwa na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara taratibu za kisheria zitakapokamilika.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















