Magazeti leo Julai 8,2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Tanzania na Qatar zimeendelea kushiurikiana kwa karibu katika sekta mbalimbali, ikiwemo masuala ya ajira ambapo tangu nchi hizo ziliposaini makubaliano ya ushirikiano wa ajira mwaka 2018 mafanikio makubwa yameonekana katika kuongezeka kwa fursa za ajira kwa Watanzania.
Aidha, amesema kupitia diplomasia ya uchumi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Watanzania wengi wameendelea kunufaika na fursa za ajira katika soko la ajira la nchini Qatar.

Mhe. Sangu amesema hayo Julai 7, 2026 jijini Doha, nchini Qatar wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukutana na Waziri wa Kazi wa Qatar Mhe. Dkt. Ali bin Samikh Al Marri ili kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo.

Amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, kwa kushirikiana na Chama cha Wakala Binafsi wa Ajira, zaidi ya vijana 9,500 wameunganishwa na fursa mbalimbali za ajira ndani na nje ya nchi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya kuongeza ajira zenye tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here