NA DIRAMAKINI
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 5 Februari 2026, limefanya uchaguzi wa wajumbe wa Kamati na Mabaraza mbalimbali ya Uwakilishi wa Bunge katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, ambapo wabunge kadhaa wamechaguliwa kuwakilisha nchi katika taasisi hizo muhimu.
Katika uchaguzi wa Tume ya Utumishi wa Bunge, wajumbe wafuatao walichaguliwa:
1:Dkt. Dotto Mashaka Biteko
2:Charles Mahela
3:Dkt. Catherine Joackim
Kwa upande wa Bunge la Afrika (PAP) – Bara, wajumbe waliochaguliwa ni:
1:Lulu Mwacha-kura 290
2:Mariam Mungula-kura 280
3:Joshua Nassari-kura 280
Katika Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC PF) – Bara, wajumbe waliochaguliwa ni:
1:Profesa Joyce Ndalichako
2:Lutengano Mwalwiba-kura 270
3:Mwanahamisi Munkunda-kura 290
Aidha, kwa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) – Bara, wajumbe waliochaguliwa ni:
1:Pindi Chana-kura 283
2:Fatma Rembo-kura 276
3:Elibariki Kingu-kura 285
4:Asha Ferouz-kura 267
5:Rashid Shangazi-kura 290
5:Kiza Mayeye-kura 251
Kwa upande wa Jukwaa la Nchi za Maziwa Makuu-Bara, wajumbe waliochaguliwa ni:
1:Silvia Sigula-kura 286
2:Ezra Chiwelesa-kura 286
3:Cosmas Bulala-kura 255
4:Bakari Shingo-kura 242
Uchaguzi huo ni sehemu ya jitihada za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuimarisha ushiriki wake katika masuala ya kikanda na kimataifa, pamoja na kuendeleza diplomasia ya Bunge kwa maslahi mapana ya taifa.
