Kamati ya Kitaifa ya NCASC yakutana Dar kujadili Usalama wa Usafiri wa Anga

DAR-Kamati ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri wa Anga (NCASC) imefanya kikao chake cha 64 jijini Dar es Salaam, Februari 3, 2026 katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayohusiana na usalama wa usafiri wa anga nchini.
Kikao hicho cha siku moja kimeongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi na kimehudhuriwa na wajumbe wa Kamati hiyo kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na Usalama wa Usafiri wa anga nchini.
Kamati hiyo ya Kitaifa ina jukumu jukumu la kuishauri Serikali katika masuala ya kiufundi, sera na hatua za kuboresha usalama wa usafiri wa anga nchini, pamoja na kuhakikisha kuwa shughuli zote za usafiri wa anga zinazingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here