BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewataka viongozi wapya wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kuwa wabunifu ili kukuza vipaji vya vijana na kurejesha heshima ya mchezo huo nchini.
Akizungumza Februari 11, 2026, katika hafla ya makabidhiano ya vifaa iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Afisa Michezo wa BMT, Apansia Lema, amesema viongozi hao wana jukumu la kuinua kiwango cha netiboli kwa kuhamasisha ushiriki wa wasichana na kuibua vipaji mikoani kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa CHANETA, Stella Mwangomale ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake kuimarisha mchezo huo huku aliyekuwa mwenyekiti, Dk. Devotha Marwa akiwataka kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ili netiboli iendelee kuitangaza Tanzania.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















