Mkuu wa Pwani, Abubakar Kunenge, ameipongeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani kwa kuiwezesha Serikali kufidiwa kiasi cha shilingi milioni 707 baada ya kumalizika kwa mashauri nane (8) ya uhujumu uchumi yaliyohusisha uharibifu wa miundombinu ya umeme na reli ya SGR mwaka 2025.

Alitoa pongezi hizo Februari 2, 2026, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kwa Mkoa wa Pwani, yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kibaha mkoani humo.
Aidha, aliipongeza Mahakama kwa mchango wake katika kukuza uchumi na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwemo kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kupitia kupunguza migogoro ya ardhi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


































