Magazeti leo Februari 5,2026

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, jana Februari 4, 2026, imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ulihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ambapo Tume ilijadili chanzo cha matukio hayo, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pamoja na mapendekezo ya kuyazuia yasijirudie.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali yakiwemo waathirika wa matukio hayo katika mikoa tofauti, ambapo Dodoma shughuli zinafanyika katika Ukumbi wa Takwimu, Iringa katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na Shinyanga katika Ukumbi wa Manispaa ya Kahama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here