Magazeti leo Februari 8,2026

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025,tarehe 6 Februari, 2026 imeendelea kukutana na viongozi na wananchi wa makundi mbalimbali, ambapo leo imekutana na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.
Kikao hicho cha pamoja kati ya Tume na Waziri Mkuu Mstaafu kililenga yaliyojiri katika kipindi cha uchaguzi Oktoba 29, ambapo vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ulitokea .

Kwa sasa Tume bado inaendelea kukusanya taarifa hizo kwa lengo la kuziwasilisha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya utekelezaji wa kudhibiti vitendo hivyo visitokee tena nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here