Malezi ya vijana yaanzie kwenye mafundisho ya Qurani-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa vijana kuisoma, kuihifadhi na kuzingatia mafundisho ya Qurani Tukufu ili kujenga kizazi chenye maadili, hofu ya Mwenyezi Mungu na mchango chanya kwa jamii.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Februari 22,2026 katika Mashindano ya Kitaifa ya Qurani Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu Foundation, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha washiriki kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza taasisi hiyo pamoja na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuendeleza mashindano hayo, akieleza kuwa ni jukwaa muhimu la kukuza vipaji na kuimarisha msingi wa kiimani kwa vijana.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza waumini kuongeza juhudi katika ibada ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendeleza matendo ya huruma na ukarimu kwa wahitaji.

Katika mashindano hayo, Said Rashid Bakari kutoka Dar es Salaam ameibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha kuhifadhi Juzuu 30 na kutunukiwa shilingi milioni 5. Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa Tuzo Maalum kwa heshima ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambapo Rais Dkt. Mwinyi alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya familia.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mhe.Mama Mariam Mwinyi, viongozi wa dini, wadhamini na wananchi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here