Naibu Waziri Maghembe akutana na Balozi wa Cuba nchini,Mheshimiwa Yordenis Vera

DAR-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru J. Maghembe (Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera, katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar Es Salaam tarehe 10 Februari, 2026.
Mazungumzo hayo yamefanyika ili kujadiliana namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba zimekuwa na uhusiano wa karibu na kindugu zaidi ya miongo sita iliyopita.
Uhusiano wetu umejengwa tangu enzi za kupigania uhuru ambapo viongozi waasisi wa mataifa yetu, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Fidel Castro wa Cuba, ambao walijenga msingi wa uhusiano, usawa na maendeleo ya pamoja.
Kwa pamoja viongozi hao, wamejadiliana namna bora ya kuendeleza ushirikiano wa uwili na kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili.Tanzania na Cuba zilianzisha ushirikiano wa kidiplomasia mwaka 1962.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here