Magazeti leo Julai 10,2026

Taasisi ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara kwa Njia Mbadala Tanzania (TIArb) imewataka wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) ili kupata elimu kuhusu njia mbadala za kutatua migogoro ya kibiashara kwa haraka, gharama nafuu na kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza Julai 9, 2026 kwenye maonesho hayo, Rais wa TIArb, Adereckson Njunwa, amesema taasisi hiyo imejitolea kuhamasisha matumizi ya usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala kama njia bora ya kupunguza migogoro inayochukua muda mrefu mahakamani na kuathiri shughuli za biashara na uwekezaji.

Amesema moja ya majukumu makuu ya taasisi hiyo ni kusimamia na kukuza utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kuandaa wataalamu wa usuluhishi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia mfumo huo katika kushughulikia migogoro yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here