DAR-Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (Primary School Leaving Examination-PSLE) utakaofanyika mwezi Septemba,2026.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, ratiba hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuwezesha wanafunzi, walimu na wadau wa elimu kufanya maandalizi ya mapema kuelekea mtihani huo muhimu wa kitaifa.
