Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edith Swebe amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Sajenti wa Jeshi la Polisi Faustina Kunjumu, ambaye amemaliza muda wake wa utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Hafla hiyo imefanyika kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wa Sajenti Kunjumu katika kulijengea Jeshi la Polisi heshima na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi wakati wa kipindi chake chote cha utumishi.
Kamanda Swebe amepongeza nidhamu, uadilifu na kujituma kwa Sajenti Kunjumu, akisema kuwa maadili aliyoonyesha yanapaswa kuwa mfano kwa askari wengine waliopo kazini na wanaoendelea na majukumu yao katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














