Profesa Mkenda ateua Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitatu

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolph Faustine Mkenda (Mb.), kwa mamlaka aliyopewe chini ya Kanuni ya 19 (2) ya Jedwali la Kwanza, Sehemu ya Tatu ya Kanuni za Chuo Kikuu Mzumbe za Mwaka 2007, ameteua Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari 14, 2026 hadi Januari 13,2029.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Lulu Mussa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Profesa Mkenda amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitatu;

i. Prof. Aloys Ntaturo Mvuma-Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
Mbeya;

ii. Eng. Bernard Boniface Kavishe-Afisa Mtendaji Mkuu na Msajili wa Bodi ya Usajili wa
Wahandisi;

iii. Bw. Juma Seleman Mkomi-Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora;

iv. Prof. Carolyne I. Nombo-Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;

v. Dkt. Morice Daudi Tegeje-Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu
Mzumbe;

vi. Bi. Nsikwa Emmanuel Chisalala-Mwakilishi wa Wafanyakazi waendeshaji, Chuo Kikuu
Mzumbe;

vii. Dkt. Zuwena Kilugwe Khamis-Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi, Tawi la Chuo
Kikuu Mzumbe;

viii.Dkt. Wilhelm Leonard Mafuru- Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti wa Kilimo, Wizara ya
Kilimo

ix. CPA. Zaina Thabit Mohamed-Meneja wa Mipango na Masoko; Bodi ya Filamu Tanzania.

x. Bw. Meshack Joram Anyingisye-Kamishna wa Bajeti; Wizara ya Fedha na

xi. Bw. Samwel Nyagawa Chacha-Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe.

"Menejimenti na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe, tunawapongeza wote walioteuliwa na tunawaahidi ushirikiano katika kufanikisha malengo ya chuo."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here